ZANTEL, BAKWATA WAZINDUA HUDUMA MPYA YA “ZANTEL MADRASA JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi. (Katikati) ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry ambaye alikuwa mgeni rasmi na Mkuu wa Itifaki BAKWATA Mohammed Nassor.


 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Hamza Zuheri.



 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.



Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel ikiwa ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.


 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Bw. Hamza Zuheri.



Mwandishi wa gazeti la The Citizen Alawi Masare (Kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Zantel Rukia Iddi Mtingwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.


Waumini  wa dini ya Kiislamu sasa watajifunza masuala ya dini kupitia simu za mkononiZantel kwa kushirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) imezindua huduma mpya inayojulikana kama ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi.

Huduma hiyo itajumuisha mambo mbalimbali kama vile Hadithi, Quran, Dua na huduma nyingine nyingi kupitia ‘App’ kwenye simu ya smartphone ((IVR/SMS/Mobile App and Bakwata News), ambapo pia mteja ataweza kupata taarifa kwa kupiga simu.

Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema, “Tunafuraha kuzindua huduma hii ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawaunganisha waumini wa dini ya Kiiislamu nchini na kuwawezesha kupata maarifa ya dini hiyo kwa urahisi zaidi.”

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa BAKWATA, Mufti Abubakar Zuberi ambae alikua mgeni rasmi alisema, “Hii ni huduma ya kipekee kwa jumuiya ya Waislamu na kila mtu anayependa kujifunza kuhusu dini ya Kiislamu. Nawaomba Waislamu wenzangu kutumia fursa hii mpya na mjiunge kwa wingi ili kujua mambo yanayopaswa kufanywa katika Uislamu.”

“Ninaamini kwamba huduma hii mpya itarahisha kazi kwetu viongozi wa Kiislamu kwa kuwa mafundisho mengi yatakuwa yanapatikana kupitia Zantel Madrasa,” alisema.

Aliongeza kwamba BAKWATA itaisaidia Zantel kuitangaza huduma hiyo hapa nchini Tanzania hususan katika misikiti.

Zantel Madrasa ni huduma ya kwanza kuzinduliwa kwenye mitandao ya simu nchini Tanzania ikilenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha watu kujifunza kuhusu dini nchini.
Huduma hii inatoa fursa kwa Waislamu wote kujiunga na huduma hii kwa kupitia namba maalumu za mtandao wa Zantel, hivyo kuwezesha watumiaji wa simu zaidi ya milioni 1 kupata mafunzo ya Madrasa kwa siku.

Watumiaji wa mtandao wa Zantel ambao watapenda kuitumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo utakayopewa ili kuunganishwa na kufurahia huduma hii.

(Picha zote na habari kwa msaada wa Michuzijr.blogspot)

Comments