Ziara ya shoo za kimuziki za msanii wa Bongo Flava nchini Tanzania huko Afrika ya Kusini, Ali Kiba zimeonyesha kuzaa matunda baada ya kuwafahamisha mashabiki wake kupitia mtandao wa instagram kuwa amekwisha kamilisha kurekodi wimbo na msanii mkongwe wa nchini humo aliyevuma miaka ya 90, Bi. Yvonne Chakachaka.
Kupitia mtandao huo, Ali Kiba aliweka picha mbalimbali zikimuonyesha na Malkia huyo wa muziki barani Afrika, kwamba amefurahi na anashauku kubwa ya kitu walichokifanya pamoja, na kumshukuru sana kwa ushirikiano huo.
Yetu sisi ni masikio kusubiria ladha tamu ya muziki uliopikwa pindi utakapoachiwa, tunaamini kitakuwa ni kitu cha kusisimua kukisikiliza na tunasubiria kwa hamu.
Comments
Post a Comment