TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA NAMNA MANCHESTER UNITED WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA WA EFL




Siku ya jana ilikuwa ni fainali ya kombe la ligi ya Uingereza au EFL Cup kama linavyojulikana ambapo ilizikutanisha timu za Manchester United na Southampton katika uwanja wa Wembley.

Katika fainali hiyo Mashetani Wekundu hao waliweka historia kwa kuwa klabu pekee nchini Uingereza kwa kuchukua idadi kubwa ya vikombe ambavyo ni 42 ikiipiku Liverpool yenye vikombe 41, zikifuatiwa na Arsenal (29), Chelsea (21) na Villa (20).



Vilevile kocha wa Man Utd, Jose Mourinho aliweka rekodi kwa kuwa kocha pekee kunyakua kikombe kwenye kila msimu wa kwanza kwa kila timu anayohamia kuifundisha.



Shujaa wa Man Utd alikuwa ni Mswiden, Zlatan Ibrahimovic aliyeifungia timu hiyo goli la kuongoza dakika ya 19 na la ushindi dakika za lala salama (87), huku Jesse Lingard akipachika goli la pili dakika ya 38.



Hata hivyo ushindi huo haukuwa rahisi kwani Southampton waliweza kurudisha goli la kwanza dakika moja kabla ya kwenda mapumziko ya kipindi cha kwanza, dakika ya 45 na kusawazisha na kufanya matokeo 2-2 dakika ya 48, yote kupitia kwa mshambuliaji wa kiitaliano, Manolo Gabbiadini.  

Kama ulikosa fursa ya kutazama shamrashamra za ushindi huo, nimekuwekea picha hapa chini:











Comments