Mwaka 2017 unaweza ukawa ni wa Diamond Platnumz kuiteka 'MAREKANI'

Mwaka 2017 unaweza ukawa ni wa Diamond Platnumz kuiteka 'MAREKANI'



Imeandikwa na kuandaliwa na Trend

Haina ubishi kuwa kwa miaka miwili iliyopita mwanamuziki wa Bongo Flava anayeipeperusha vema bendera ya muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania kimataifa, Diamond Platnumz au 'SIMBA' kama anavyopenda kuitwa na mashabiki wake aliliteka vilivyo bara la Afrika.

Juhudi za kuliteka bara la Afrika lilifanikiwa kwa mikakati kabambe ambayo alijiwekea kwa kuanza kuwashirikisha wasanii wa nje ya ukanda wa Afrika ya Mashariki, hususani Nigeria na Afrika ya Kusini ambao wao wamekwishavuka mipaka tayari huku wakiwa na mashabiki lukuki.

Wimbo wa Number One Remix' aliomshirikisha  Davido ndio ulianza kwa kufungua milango ya 'Kolabo' kali za wasanii wa kiafrika mpaka leo hii tunapozungumza tayari hewani ana ngoma kali na msanii wa RnB kutoka Marekani, NEYO.

Hatua aliyoipiga msanii huyu ni dhahiri kwamba ukuaji wake unaenda kwenye grafu nzuri na iliyopangiliwa, yaani kuiteka Tanzania nzima, Afrika ya Mashariki na Kati, Kusini, Magharibi na hatimaye nje ya bara la Afrika kabisa.

Kama unadhani ninakutania kwamba mwaka huu unaweza kuwa ni wa kuiteka MAREKANI shauri yako kwa sababu tayari blogu ya 'THIS IS 50' inayomilikiwa na msanii wa HIP-HOP wa nchini humo tayari amekwishaipa shavu video ya wimbo huo.

Kama hujawai kuona video hiyo, tafadhali tazama hapa chini na kisha uone juhudi unazozifanya mtanzania huyu katika kuufikisha muziki wake na wa nchini kimataifa.




Comments