INSTAGRAM ITAKUWEZESHA KUWEKA PICHA NA VIDEO MPAKA 10 KWA WAKATI MMOJA


Kama ulikuwa unashindwa kuwashirikisha rafiki zako picha na video nyingi kwa pamoja ndani ya wakati mmoja kupitia kwenye ukurasa wa mtandao wako wa Instagram basi hali hiyo haitokuwepo tena kwani jana siku ya Alhamisi, mtandao huo walitambulisha kipengele kipya.

Mapema mwezi huu, mtandao unaowawezesha watu kuwashirikisha picha wenzao, Instagram, ulikuwa ukifanyia majaribio kipengele kipya kupitia programu ya 'Android' kwa watumiaji wachache waliochaguliwa. Kipengele hicho kipya kitatambulishwa rasmi kwa watumiaji wa 'Android' na 'iOS' wiki chache zijazo.

"Sasa utaweza kuweka picha na video mpaka 10 katika 'post' moja na kuzitazama zote," ilisema Instagram kwenye sehemu ya taarifa kwa waandishi wa habari.

Ili kuendana na matumizi ya watumiaji, Instagram imeongeza uwezo na urefu wa picha na video mpaka 10, tena zikiwa zenye muonekano tofauti.

Hapo awali ni wenye matangazo ya biashara tu ndio waliokuwa na uwezo wa kuweka albamu ya picha zao huku watumiaji wengine wakiwa na fursa ya kuzitazama, lakini sasa mtandao huo umewafungulia njia watumiaji wake zaidi ya milioni 600 kufanya hivyo.

Ili kuweka picha nyingi, watumiaji wanaweza kuchagua mpaka picha 10 kutoka kwenye albamu zao, kuweka urembo au madoido kwenye picha wanazozitaka, kisha kuzishirikisha kwa wengine wazione kupitia kurasa zao.

Kutoka kwa watu wanaowafuatilia, wataiona hiyo albamu ya picha, wakaziperuzi na kuweka alama ya kuzipenda wakati wakiendelea kuziangalia.     

Kwa uelewa zaidi tazama video niliyokuwekea hapo chini, nadhani utakuwa unasubiria kwa hamu huduma hiyo ianze kufanya kazi:

  

Comments