HII HAPA NI DROO YA EUROPA LEAGUE HATUA YA 16 BORA

UEFA EUROPA LEAGUE imeweka wazi timu zitakazokutana kwenye hatua ya 16 bora huko barani Ulaya.

Katika droo hiyo timu ya Manchester United itamenyana na Rostov inayoshiriki ligi kuu ya Urusi, ambayo ndiyo pekee iliyofanikiwa kutinga hatua hiyo kutoka kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya Tottenham jana kutolewa baada ya kulazimishwa suluhu na Gent ya Ubelgiji.

Watanzania tumekuwa na bahati katika kombe hilo kwa kuwakilishwa na Mtanzania Mbwana Alli Samatta ambaye anakipiga nchini Ubelgiji timu ya Genk, wao wamepangiwa timu ambayo nayominatokea katika ligi hiyo hiyo, Gent.

Kwa kujua timu zote zilivyopangwa, nimekusogezea ratiba kamili kama ilivyowekwa wazi na waandaji wa kombe hilo UEFA EUROPA LEAGUE kupitia mtandao wao rasmi wa ukurasa wa Twitter. KARIBU




Comments