Kampuni ya mkononi ya Airtel Kwa kushirikiana na Tecno mobile leo imewazawadia wateja wake kupitia promosheni iliyozinduliwa maalumu kwa msimu wa sikukuu za crismass, mwaka mpaya na valentine kwa lengo la kuwahamasisha wateja kutumia simu za kisasa za smartphone na kujishindia
Promosheni hiyo ilihusisha wateja wa Airtel wanaonunua simu aina ya TECNO N6 and TECNO W3 kwa kipindi cha sikukuu za krismasi, mwaka mpya na valentine na kisha kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia vifaa mbalimbali vya nyumbani vikiwemo , Televisheni, Mashine ya kutengenezea Juisi, Jiko la kuchoma nyama, Mashine ya kutengeneza Sandwich , Brenda mashine pamoja na simu za smartphone za TECNO W4 mbili
Akiendesha droo hiyo iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “Airtel tuefika mwisho wa promosheni yetu lakini bado smartphone zinapatikana katika maduka yetu zikiambatana na ofa kabambe. Napenda kuwashukuru wote walijiunga na ulimwengu wa smartphone kupitia promosheni hii nakuwaomba wateja wetu wengine waendelee kutembelea maduka yetu ili kupata simu za kisasa kwa bei nafuu na kufurahia huduma zetu bora ikiwemo, Airtel Money Relax, huduma ya Inteneti na nyingine nyingi”
Kampuni ya Airtel ilizindua promosheni ya shinda na Smartiphone mwishoni mwa mwaka jana ili kila mteja wake anaenunua simu aweze kupata nafasi ya kushinda.
Comments
Post a Comment