Imeendikwa na Trend
Mara nyingi wasanii huwa wanapotambulisha nyimbo mpya huwa wanaachia ya kusikiliza 'audio' pamoja na ya kuona 'video' ili kuwateka wapenzi wa aina zote.
Lakini hilo lilikuwa tofauti kwa msanii wa kike anayefanya vizuri nchini kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava, Dayna Nyange ambaye amepetamba na nyimbo kadhaa kama vile Nivute kwako, Angejua, Fimbo ya Mapenzi na nyinginezo.
Msanii huyu aliuachia wimbo wake wa 'KOMELA' aliomshirikisha Rapa mkali kwa sasa, Billnass takribani miezi 6 iliyopita, tofauti na watu walivyotarajia kama angeutoa pamoja na video yake.
Hakuna anayeweza kukataa kwamba huu wimbo ni mkali na umekuwa maarufu masikioni mwa watu na kuteka hisia zao. Ninaamini kuwa kuachiwa kwa video yake kunaweza kuurudisha tena kwenye macho pamoja na masikio ya watu, hivyo kuupatia maisha marefu zaidi kwenye mzunguko wa vyombo mbalimbali vya habari.
Nisikuchoshe kwa maneno mengi, hebu itazame 'video' ya wimbo huo hapo chini na kisha toa maoni yako ni nini unafikiria.
Comments
Post a Comment