Jana kupitia kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE au maarufu kama FNL kinachorushwa na kituo cha TV cha EATV ilibidi awepo msanii wa muziki wa bongo flava kutoka lebo ya muziki ya WCB, Harmonize kwa ajili ya kutambulisha video yake mpya ya "NIAMBIE."
Hayo ilibidi kufanyika muda mfupi tu baada ya msanii mpya kwa anga ya muziki wa bongo flava na asiyeishiwa vituko, Harmorapa, kumaliza mahojiano yake.
Lakini cha kushangaza kilichotokea ni pale Harmonize alipogoma kuingia ndani na kuishia nje ya studio tena hata hakushuka kutoka kwenye gari lake. Msanii huyo alifanya hivyo baada ya kumuona bosi anayesimamia kazi za msanii Harmorapa, Bi. Irene Sabuka.
Kwa mujibu wa msanii Harmorapa na msanii mwingine wa lebo aliyopo msanii huyo ya SGS SABUKA MUSIC, KILORITI, wamesema kwamba Harmonize hakushuka kutoka kwenye gari lake baada ya kumuona Irene na badala yake alishusha kioo cha gari na kumuonyesga bosi huyo kidole cha "KATI."
Hali hiyo ilitafsiriwa kwamba Harmonize alidhani kwamba ameitwa kwenye kipindi hicho ili kuhojiwa pamoja na Harmorapa, msanii ambaye ametoka kwa kupitia kiki ya kujifananisha na msanii huyo, kitu ambacho inasemekana Harmonize hajakipenda na kufikia hatua mpaka msanii mwenzake, "DANCER" kutoka WCB, Moze Iyobo kumfananisha na "NYANI."
EATV waliweka wazi kuwa hawakumuitia Harmonize kwa ajili ya kuja kumkutanisha na msanii Harmorapa au kumpambanisha naye kama inavyochukuliwa mtaani badala yake kuja kutambulisha rasmi video yake ya "NIAMBIE" ambayo aliachia tu bila ya kufika studio kama huwa anavyofanya mara nyingi.
Lakini EATV wameahidi kuwa msanii Harmonize atakuwepo kwenye kipindi kijacho siku ya Ijumaa ya tarehe 31/03/2017.
Cheki video ya Harmorapa hapa chini aliyomshirikisha JUMA NATURE ambayo kwa sehemu kubwa anamchana MOZE IYOBO na wasanii wa kundi la WCB.
Comments
Post a Comment