UINGEREZA NA UJERUMANI KUSHUKA DIMBANI LEO




Timu ya taifa ya Uingereza leo usiku majira ya saa 4:45 usiku itakuwa ugenini katika uwanja wa Signal Iduna Park kumenyana na Ujerumani katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza wa kimataifa chini ya kocha Gareth Southgate ambapo atamkosa nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ambaye ameondolewa kwenye kikosi hiko kutokana majeraha ya goti huku nafasi yake ikichukuliwa na Gary Cahill.


Timu hiyo bado haijaonja kipigpo chini ya kocha huyo na watakuwa kwenye kipimo kingine cha kuendeleza ushindi dhidi ya timu hiyo ambapo mara mwisho walipokutana waliifunga Ujerumani magoli 3-2.


Kikosi cha Uingereza kitaundwa na wachezaji; Joe Hart, Kyle Walker, John Stones, Gary Cahill, Ryan Betrand, Eric Dier, Alex Oxlade-Chamberlain, Adam Lalana, Raheem Sterling, Dele Alli na Jamie Vardy. 

Huku Ujerumani wao watakuwa bila ya kipa wao nambari moja Manuel Neuer ambaye naye pia ni majeruhi, kikosi chao ni; Marc-Andre ter Stegen, Joshua Kimmich, Antonio Reudiger, Niklas Suele, Jonas Hector, Emri Can, Julian Weigl, Leroy Sane, Julian Draxler, Lukas Podolski na Timo Werner.


Mechi zingine za kutazama usiku wa leo ni pamoja na Scotlanda dhidi ya Canada saa 4:45 usiku na Czech Republic dhidi ya Lithuania saa 2 usiku.       

Comments