MATOKEO YA UEFA, EUROPA LEAGUE NA LA LIGA

Jana siku ya Jumatano ya Februari 22, 2017 zilichezwa mechi kadhaa barani Ulaya zikiwemo KLABU BINGWA, KOMBE LA EUROPA LEAGUE pamoja na LA LIGA.

Mechi za Klabu Bingwa zilizikutanisha timu za FC PORTO ya Ureno na JUVENTUS ya Italia ambapo JUVENTUS ilijiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwa kuibuka na ushindi wa magoli mawili kupitia kwa wachezaji, Marco Pjaca na Dani Alves dakika za 72 & 74.


Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Sevilla ya Hispania na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, Leicester City, mchezo ambao ulimalizika kwa Sevilla kushinda magoli 2-1, magoli yaliyoshindwa na Pablo Sarabia na Joaquin Correa dakika ya 25 & 62, huku goli la Leicester City la kufutia machozi likifungwa na Jamie Vardy dakika ya 73.



Vilevile mashetani wekundu kutokea Uingireza, timu ya Manchester United wao nao walisafiri mpaka Ufaransa kwenda kumalizia mkondo wa pili wa Ligi ya Europa dhidi ya St. Etiene ambapo awali waliwafunga magoli 3-0 walipowatembelea nyumbani kwao kwenye uwanja wa Old Trafford. Katika mechi hiyo mchezaji Henrikh Mkhitaryan aliifungia Man Utd goli pekee mnamo dakika ya 17 na hivyo kuwafanya kumaliza mizunguko yote miwili kwa jumla ya magoli 4 na hivyo kusonga mbele hatua ya 16 bora. Katika mechi hiyo beki wa Man Utd Eric Bailly alitolewa kwa kadi nyekundu huku Mkhitaryan akitolewa nje kwa maumivu ya misuli.  


Huko nchini Hispania kwenye Ligi ya La Liga, kiporo kiliwachachia mabingwa watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya, Real Madrid baada ya kulala kwa magoli 2-1 dhidi ya Valencia, magoli ya Valencia yalifungwa ndani ya dakika 5 na wachezaji yaliyofungwa Simone Zaza na Fabian Orellana dakika za 4 & 9, huku Cristiano Ronaldo akifunga goli dakika ya 44 na hivyo kuifanya Real Madrid kubakiza kiporo cha mechi nyingine moja na kuwa kileleni kwa alama moja nyuma ya Barcelona.



Comments