Baada ya kimya cha muda mrefu kutoka kwa msanii ROMA MKATOLIKI baada kukumbwa na masahibu ya kutekwa pamoja na wasanii wenzake wakiwa katika studio za Tongwe Records hatimaye ameachia wimbo mpya.
Kwenye wimbo huu msanii huyo wa hip-hop ambaye siku zote mistari yake huwa inaangazia masuala mbalimbali yanayotukia kwenye jamii kwa kiasi kikubwa amezungumzia tukio la kutekwa kwake, mambo yaliyozungumzwa na yeye mwenyewe alivyolichukulia tukio lile.
Hii hapa ni video ya wimbo huo ikiwa imefanywa na muongozaji Nicklass hukua audio ikifanywa na Bin Laden wa Tongwe Records ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa waliotekwa:
Comments
Post a Comment