VIDEO: Ben Pol ft Mr. Eazi - Phone

VIDEO: Ben Pol ft Mr. Eazi - Phone



Imeandaliwa na kuandikwa na Trend

Msanii Ben Pol ametuletea video ya wimbo wake wa 'Phone' iliyofanywa na watayarishaji Tiddy Hotter kwa upande wa 'audio' na Hanscana kwa 'video'. Katika wimbo huu msanii kutoka nchini Nigeria lakini alikuwa akifanyia shughuli zake nchini Ghana tangu mwaka 2007 ambapo tayari amekwisharejea takribani miaka miwili iliyopita.

Katika 'video' Ben Pol anaonekana kama vile anaingia nyumbani kwake na kumkuta msichana mrembo, bila ya shaka ni 'girlfriend/mke' wake akiwa anafanya kazi zake kwenye 'laptop'. Anaweka simu yake ya mkononi mezani, wanasalimiana kimahaba na kisha anatoka. Bila ya kujua anatoka eneo lile na kuisahau simu ile mezani, na hapo ndipo balaa lililomfanya mpaka aimbe wimbo huu ndo linaanza.



Ukitazama mbele zaidi kwenye hii 'video' ataonekana msanii Mr. Eazi, kama kawaida yake akiwa ameivalia kofia shingoni na kuitupia mgongoni ikining'inia. Anaonekana akiwa na Ben Pol wakitembea na kupiga 'story' katika hoteli iliyopo pembezoni mwa ufukwe wsa bahari.

Video ni nzuri na imefanywa katika mazingira tofauti ambayo yatayavutia macho yako kuingalia, bila ya kusahau simulizi nzuri kutoka kwa wasanii hawa walioshirikiana kulalama juu ya 'SIMU' zao kushikwa na kukaguliwa na wapenzi wao bila ya ridhaa yao. Sasa sidhani kama katika mahusiano ya sasa hivi mnaweza kuishi bila ya kufanya hivyo.

Itazame hiyo 'video' hapa chini kujionea mengi zaidi kutoka kwa muongozajia ambaye kwa kweli anastahili pongezi kwa ubunifu ambao anaoufanya katika kila kazi anayoifanya. KARIBU!



   

Comments