INAWEZEKANA G NAKO ALIKOPI NGOMA YAKE YA "GO LOW" KUTOKA KWA MSANII HUYU??????

Baada ya msanii wa kundi la WEUSI kutokea mkoani Arusha, G Nako kuachia ngoma yake mpya ya "GO LOW" iliyotengenezwa na mtayarishaji wa muziki Luffa ambaye kwa sasa yupo chini ya uongozi wa studio za WANENE ENTERTAINMENT, yaliibuka maswali mengi kwamba ame-kopi 'idea' kutoka kwa msanii Flowking Stone ambaye anatokea nchini Ghana.

Flowking Stone yeye naye ana wimbo wake unaokwenda kwa jina hilo hilo la "GO LOW" ambao aliuchia mwaka 2016, hebu itazame hapa na kuisikiliza vizuri pamoja na kuilinganisha na ile aliyoifanya G Nako ambayo haina hata wiki mbili tangu aichie na utafakari kama kwa namna moja ama nyingine mawazo yaligongana???




Comments