50 CENT ACHOMOA KUSHIRIKI "PARTY TOUR" YA CHRISS BROWN


Msanii wa Hip-Hop kutokea nchini Marekani, 50 Cent amemtolea nje Chriss Brown kushiriki kwenye ziara yake itakayokwenda kwa jina la "PARTY TOUR" kwa kile alichodai kwamba promota hakuweza kumudu kumlipa.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, 50 hakukamilisha mkataba. Alitakuwa kuongoza kwa upande wa wageni wa waalikwa kwenye "tour" hiyo baada ya upande wa Chriss Brown kukubaliana malipo. Promota wa shoo hiyo, Live Nation alikuwa tayari amekwishamjumuisha msanii huyo kwenye matangazo lakini mambo yalikuja kubadilika wakati wa makubaliano ya mwisho ambapo walitofautiana kwa kiasi kadhaa cha fedha.

Taarifa zinadai kuwa 50 Cent alikwishawakatalia tangu wiki mbili zilizopita huku matangazo yakiwa yamekwishaenda hewani wiki moja kabla. 

Kupitia ukurasa wake wa instagram alipost picha na maneno yanayosomeka, "Nisingeweza kusema kuwa marafiki zangu hawawezi kumudu kunilipa mimi. Bali hii kitu hakikuweza kushughulikiwa ipasavyo, Bado niko narekodi sehemu za filamu yangu ya 'Den of Thieves'.

50 Cent si msanii wa kwanza kujitoa kushiriki kwenye shoo hiyo bali tayari French Montana ambaye anaye alikuwa tayari amekwishajumuishwa kwenye matangazo alijitoa pia.

Lakini hiyo haimzuii Chriss Brown kuendelea na shoo yake ya "PARTY TOUR" kwani kuna wasanii wengine kadhaa watakaojumuika naye wakiwemo Fabolous, O.T. Genasisi na Kap G.

Comments