Tigo Tanzania kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach for Change imetoa tuzo ya dola za Marekani 20,000 kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la tano la Kidijitali la Tigo la waleta mabadiliko (Tigo Digital Changemakers). Shindano hilo linalenga kuibua na kuwasaidia wajasiriamali jamii ambao wanatumia programu na teknolojia katika kuboresha jamii na kuleta mabadiliko kwa vizazi vijavyo. Pamoja na nyongeza katika msaada huo wa kifedha, washindi wanapewa nafasi ya kutumia kituo cha Reach for Change ambacho kinawapatia ushauri, utaalamu na kuingia katika mitandao duniani ambayo itawawezesha kujenga ujasirimali jamii ulio endelevu kifedha utakaounda mabadiliko katika uwanja mpana.
Washindi wa mwaka huu katika tuzo hiyo ni Sophia Mbega na Nancy Sumari. Sophia Mbega aliwavutia majaji na mkakati wake mkubwa wa kidijitali ambao umejielekeza katika kuvisaidia vikundi binafsi vya wanawake maarufu kama VICOBA. Ameibuka na programu ya simu ambayo inaunda jukwaa la ushirikiano linalotumia programu zilizopo kwa usimamizi wa kifedha na majukumu katika njia ambayo inaendana na mazingira ya Kiafrika. Kupitia programu hiyo, watumiaji wote, bila kujali sehemu wanayokuwepo wanaweza kuhamisha fedha kwenda katika akaunti ya kikundi cha Vicoba (ikiwa ni moja kwa moja kwa kutumia namba iliyo katika mfumo wa USSD), kuangalia rekodi zao zote za kifedha, faida iliyozalishwa, taarifa za wiki n.k.
Mkakati ulioshinda tuzo wa Nancy Sumari unajulikana KIDS JENGA HUB ambao unaangalia msingi wa uelewa wa watoto. Kupitia mkakati huo wa nafasi ya kuanza kuwashirikisha watoto, anafundisha program za kompyuta, matumizi ya kiroboti na stadi za kuweka namba kwa wanafunzi wa shule ya msingi. Mkakati huo pia unawafunulia watoto katika kujifunza msingi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kama vile stadi za kiprogramu ambazo matokeo yake zinatumika katika malengo mengi ya kielimu na burudani.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Ni kutokana na furaha hii kubwa kwamba tunatangaza washindi wa mwaka huu wa Shindano la Tigo la kidijitali la Waleta mabadiliko. Kwa mwaka wa tano sasa Waleta mabadiliko wameyagusa maisha ya watoto zaidi 250,000 nchini Tanzania na tunaamini kwamba kwa nyongeza hii ya Waleta mabadiliko wawili tutaleta mabadiliko katika maisha ya watoto wengi zaidi na kusaidia kuifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri kwa vizazi vyetu vijavyo.”
Gutierrez aliendelea kufafanua kwamba kama nembo ya maisha ya kidijitali Tigo inatoa msukumo kwa mawazo na miradi inayoendeshwa na teknolojia ambayo yanaleta mabadiliko endelevu. “Teknolojia ya kidijitali sio tu inabadilisha namna ambavyo tunafanya biashara ndani ya Afrika bali pia inaleta mapinduzi kwa njia tofauti na kutatua masuala ya maendeleo ya jamii. Hivyo kutokana na heshima hii kubwa ni kwamba kwa mara nyingine tunaunda fursa kwa kwa mawazo hayo kutambuliwa, kuungwa mkono na kubadilisha hadi kiwango cha juu cha matokeo ya kijamii na kiuchumi,” alisema.
Huu ni mwaka wa tano ambapo Tigo na Reach for Change wanatangaza washindi wa shindano hilo. Washindi walioingia fainali ambao huchaguliwa kutoka kundi la mamia ya wajasirimali jamii ambao wametumia programu za kiteknolojia kupata suluhisho kwa matatizo yanayoikabilia jamii ya Watanzania.
Gutierrez aliwapongeza washindi waliotangulia na papo hapo akitoa msukumo kwa wengine kushirikiana mawazo yao.
“Uchaguzi wetu wa wajasiriamali jamii unavutia sana. Hadi sasa tumeshasaidia jumla ya waleta mabadiliko ya kidijitali jamii tisa (9) na tunatarajia kuwasaiidia wajasiriamali jamii wengine kila mwaka, ili kufanya karakati hizi zisonge mbele.”
Waleta mabadiliko katika program hi ni pamoja na Faraja Nyalandu ambaye anaendesha ujasiriamali jamii kidijitali unaofahamika Shule Direct. Shule Direct inatoa mada za kielimu kidijitali kukabiliana na uhaba wa walimu na kuhakikisha kila mtoto na vijana wanapata elimu bora. Asasi ya Faraja pia inatoa programu ya simu inayofahamika Makini SMS ambayo inawasaidia watoto kujifunza kwa kutumia maswali ya kuchagua masomo tisa. Hivi sasa amepanga kuifanya asasi hiyo kuwa ya kikanda.
Carolyne Ekyarisiima ni mleta mabadiliko ya kidijitali mwingine wa Tigo ambaye anafanyika kazi kuziba pengo la kijinsia katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia ujasiriamali wake wa kijamii, Apps & Girls. Carolyne ameleta mabadiliko kwa mamia ya watoto wa kike , kupitia klabu za masomo shule, warsha, maonesho , kuweka kambi pamoja na mashindano. Sio tu kwamba hii inasaidia bali pia inahakikisha kwamba watoto wa kike wengi wanaweza kuzifikia teknolojia za kidijitali. Hali kadhalika Carolyne amewawezesha kuwa viongozi wa Tehama wa baadaye. Carolyne hivi sasa anaupanua ujasirimali jamii wake kuleta matokeo makubwa na kuwapatia wasichana walio wengi elimu ya teknolojia na kuwasaidia kuanzisha masuluhisho kwa masuala ya kijamii kupitia kupitia programu zao za kidijitali na mitandao.
Joan Avit ni mleta mabadiliko mwingine ambaye anaboresha ubora wa elimu ya awali kupitia ubinifu wa kidijitali. Ubunifu wake unaofahamika GraphoGame Tanzania unawapatia kujifunza kupitia mchezo ambao ni rafiki kwa motto ambao unawasaidia watoto kujifunza kusoma kwa kuzitambua herufi. Ubinifu wake umebadilisha maisha kwa mamia ya wanafunzi wadogo ambao awali walikuwa na hali mbaya katika kujifunza lakini hivi sasa wanachanua kutokana na ubunifu wake wa kidijitali.
“Tumekuwa tunaunga mkono kazi zote za waleta mabadiliko wetu na mwaka huu tumeangalia na kuwaunga mkono wajasiriamali jamii wengine wawili walio jasiri na wabunifu,” alisema Gutierrez.
Akizungumza hafla ya tuzo hiyo Meneja Programu wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka alipongeza ushirikiano wa asasi hiyo na Tigo, akibainisha kwamba imetoa fursa sahihi kwa utekelezaji wa miundo ya biashara iliyoendelevu ambayo inanufaisha jamii hususani idadi kubwa ya watoto kote nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni Meneja Programu wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka na Meneja Huduma za jamii(CSR) Tigo , Halima Okash.
Meneja wa Programu wa Reach For Change, Josephine Msambichaka akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akiongea na wageni waalikwa kwenye hafla ya makabidhiano.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni Meneja Programu wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka na Meneja Huduma za jamii(CSR) Tigo , Halima Okash.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Sophia Mbega (katikati)wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni kulia Meneja Programu wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka, Halima Okash na mwisho kulia ni Nancy Sumari.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Nancy Sumari (katikati)wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni kulia Meneja wa Programu wa Reach For Change, Josephine Msambichaka na Halima Okash.
Mshindi wa shindano la Tigo Digital Changemakers,Sophia Mbega akiongea na wanahabari mara baada kukabidhiwa hundi ya dola za kimarekani elfu 20 jijini Dar Es Salaam leo, Pichani nyuma ni Mshindi wa shindano hilo pia aliyejinyakulia pesa hizo, Nancy Sumari. Jumla ya washindi wawili walipata dola elfu 20 kila mmoja.
Comments
Post a Comment