Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, Leicester City jana walifanya kile kinachoonekana ni muendelezo wa maajabu ya soka baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Klabu bingwa barani Ulaya kwa kuitoa Sevilla jumla ya Magoli 3-2.
Magoli ya Leicester yaliyofungwa na nahodha wa timu hiyo Wes Morgan dakika ya 28 na Marc Albrighton dakika chache baada ya mapumziko yalitosha kabisa timu hiyo ambayo ilimtimua kocha wake Claudio Ranieri licha ya kuipandisha daraja na kuipatia ubingwa na kumkabidhi mikoba aliyekuwa kocha msaidizi, Craig Shakespeare.
Mchezo huo ilishuhudiwa mchezaji Samir Nasri akitolewa nje kwa kadi nyekundu huku Steven Nzonzi akikosa penati na hivyo kufifisha kabisa matumaini ya timu hiyo kutokea Hispania kusonga mbele.
Katika mchezo mwingine jana usiku, miamba ya soka kutoka Italia, Juventus wao pia waliivuka hatua hiyo baada ya Paulo Dybala kushinda goli pekee kwa mkwaju wa penati na hivyo kufanya jumla ya magoli kuwa 3-0 dhidi ya FC Porto ya Ureno.
Comments
Post a Comment